The House of Favourite Newspapers

Mwili wa marehemu Gardner G Habash Wawasili Nyumbani Kwake Kijitonyama – (Video+Picha)

0
Mwili wa marehemu Captain Gardner G Habash ukiwasili nyumbani kwake Kijitonyama ambapo utafanyiwa ibada maalum ya familia leo.

Mwili wa marehemu Captain Gardner G Habash leo Aprili 21, 2024 umewasili nyumbani kwake Kijitonyama ambapo utafanyiwa ibada maalum ya familia leo, na kesho kuagwa katika kanisa la KKKT Mbezi Beach saa mbili asubuhi na baadae viwanja vya Leaders Club.

Gardner G. Habash amefariki dunia alfajiri ya Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Gardner G Habash, Kijitonyama
Katibu Mkuu wa UVCCM – Taifa, Jokate Mwegelo, akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Gardner G Habash.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha maombolezo.

Leave A Reply