The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mngereza Kuwasili Dar Leo; Ratiba Hii Hapa…

0

MWILI wa aliykuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza, unatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Desemba 28, 2020.

 

Taarifa iliyotolewa na BASATA imeeleza kuwa, mwili utaagwa Jumanne katika ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika Desemba 30, 2020 kijijini kwao Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

 

Mngereza alifariki dunia Desemba 24 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).

 

Leave A Reply