The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mngereza wa Basata Kuwasili Jumatatu

0

MWILI wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza, utawasili jijini Dar es Salaam Jumatatu Desemba 28, 2020.

Katika taarifa iliyotolewa na Basata, mwili wa Mngereza utaagwa Jumanne katika ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika Desemba 30, 2020 kijijini kwao Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Mngereza alifariki Desemba 24, 2020 katika Hospitali ya Rufaa Dodoma alikokuwa akitibiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU).

Leave A Reply