The House of Favourite Newspapers

Mwingine Mweusi Auawa kwa Risasi Marekani

0

KISA kingine cha Polisi nchini Marekani kumpiga risasi na kumuua Mmarekani mweusi katika mji wa Atlanta Georgia wikiendi hii, kimezua ghadhabu na maandamano tena, pamoja na mjadala unaoendelea ulimwenguni kote wa kupinga ubaguzi wa rangi.

Mkuu wa Polisi wa Atlanta tayari amejiuzulu wadhifa wake kutokana na kisa hicho. Kadhalika idara ya polisi ya Atlanta imesema, imemfuta kazi polisi mmoja kutokana na kifo hicho.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyetambuliwa kwa jina Rayshard Brooks alipigwa risasi siku ya Jumamosi, alipokataa kukamatwa baada ya kufeli katika vipimo vya kubaini hali yake au ikiwa ametumia mihadarati.

Kufuatia kifo chake maandamano yamezuka Atlanta na kwingineko nchini Marekani huku waandamanaji wakichoma moto mkahawa wa Wendy karibu na eneo alikouawa. Kisa hicho kimejiri wiki chache baada ya mauaji ya George Flody ambayo yalichochea maandamano makubwa ulimwenguni kote.

Leave A Reply