The House of Favourite Newspapers

Nikki wa Pili: Sifa ya Mahusiano Kufanana – Video

0

 

RAPA maarufu nchini, Nikki wa Pili amesema sifa ya kuhusiana lazima mfanane, huku akitolea mfano kuwa wanywaji wa pombe lazima watatembea pamoja, wavuta bangi vile vile na wasoma kadharika.

 

Nikki amesema hayo wakati akifanya mazungumzo na kipindi cha Darasa kinachoruka kupitia +255 Global Radio kila siku saa 10:00 hadi saa 11: jioni.

 

“Na sifa nyingine ni kwamba ukianza kufanya vizuri na kupiga hatua unakuwa umewa-outshine wenzako, ili kuzuia hilo, mahusiano yana tabia ya kutaka kila siku mbaki sawa.

 

“Mafanikio yana-attract watu, lakini je utaweza kuya-control, mtu anayekuja kwenye mahusiano yako anafahamu ulipotoka? Anaweza kuja akakutoa kwenye trap na kuku-destroy kwa sababu hajui siri ya mafanikio yako.

 

“Sisi vijana tuna culture ya kuwabeba wana, ili wewe uweze kutoka uwe mtu fulani lazima uachane na marafiki ulionao, uende kwa watu sahihi.

 

“Wakati nasoma nilikuwa namarafiki, walivuta bangi, lakini mimi nilisema no, siwezi kuvuta bangi sababu nilikuwa na ndoto zangu, kama ningeamua kukaa na grupu na kufuata waliokuwa wakifanya, leo nisingingekuwa hapa GlobalPublishers tunafanya interview.

 

“Nilichagua marafiki wazuri nilipokuwa form four, tulipangisha geto tukawa tunalipa shilingi elfu tatu. Baadaye wote tulikuja kufaulu, tukaja Dar tukaendelea na masomo na sasa wote tuna nafasi fulani, wengine wamejiriwa TRA, na mimi nipo na mambo yangu.

 

“Unaweza kuamua kuwa na geto lako, kuwa na mpenzi, kusaidia wazazi na kufanya biashara zako, njia hii ni ngumu kuliko aliyechagua kukaa mtaani na kuvuta bangi, utakuwa umebeba majukumu lakini huyu atakuwa yupoyupo tu hata jamii imemtoa kwenye majukumu.

 

“Tulianzisha Smart Generation kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika nyanja mbalimbali. Tuna project ya kuwasidia vijana na nyingine akina mama hasa kupunguza vifo vya wajawazito,” amesema Nikki wa Pili.

 

“Ili uweze kufanikiwa, lazima uangalie ni aina gani ya watu umekuwa ukihusiana nao. Mtu mwingine unaweza kuwa na uhusiano naye akakudidimiza, mwingine akakusaidia kukua na mwingine akakubakisha pale pale ulipo.

 

“Ukizungukwa na watu ambao wanakuona wewe ndio kiongozi wao, wewe ndio role modal wao, uhusiano huo inabidi uubadilishe. Inabidi uende kwa watu ambao wanakuzidi waweze kukupa changamoto na njia ya kubadilisha maisha yako,” amesema Eric Shigongo.

 

Leave A Reply