Mwinyi Amteua Masoud Makamu wa Kwanza wa Rais

OTHMAN  Masoud Othman ameteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kujaza nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alifariki dunia tarehe 17 Februari, mwaka mwaka huu jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

 

Uteuzi wa Masoud umefanywa na Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi baada ya mashauriano na chama cha ACT-Wazalendo.

 

 

Masoud amewahi kuhudumu katika nafasi za ngazi za juu katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa sasa ni mwanachama wa ACT Wazalendo.

 

 

Anatambuliwa kwa msimamo wake usioyumba wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani na nje ya nchi na pia uwezo wake mkubwa kwenye taaluma yake ya sheria.

 

Toa comment