The House of Favourite Newspapers

Mzungu Apewa Mkataba Wa Okwi

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda

 

BAADA ya timu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini kutuma barua kwa uongozi wa Simba kuhitaji kumsajili mshambuliaji wao, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, imebainika kuwa hatima ya mchezaji huyo kujiunga na timu hiyo ipo juu ya kocha mkuu Mbelgiji, Patrick Aussems.

 

Dirisha dogo la usajili la kimataifa linatarajiwa kufunguliwa mwezi Januari mwakani kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

 

Akizungumza na Championi Iju­maa, Katibu wa Simba, Dr Arnold Kashembe alisema kuwa mezani kwake kuna barua nyingi la­kini kuhusu Okwi kujiunga na timu ya Kaizer Chief ni mpaka kocha atoe maamuzi ya mwisho ndiyo wanaweza kumuachia.

 

“Mimi siwezi kuzungumzia hilo kwani kuna barua nyingi ambazo zinakuja lakini mwenye maa­muzi ya mwisho ni mwalimu ambaye kama akiafiki sisi tupo tayari lakini pia kama ikitokea taarifa yoyo­te sisi tuta­wataarifu,” alisema Kashembe.

MASHABIKI wa Simba Wacharuka Ndani ya Daladala Watu wapagawa

Comments are closed.