Mzungu Kichaa Amfagilia P Funk Kukuza Muziki Bongo – Video

Msanii wa Bongo mwenye asili ya Ulaya, Mzungu Kichaa,  akifanya mahojiano na Bongo 255.

MSANII wa Bongo mwenye asili ya Ulaya, Mzungu Kichaa, leo  Jumanne 14, 2020, amempongeza prodyuza Paul Matthysse anayejulikana kwa jina la P Funk Majani kwa mchango wake mkubwa katika muziki wake (Mzungu) na kumfanya aeleweke katika jamii ya Tanzania kupitia ngoma yake ya ‘You Got Me’ na nyinginezo katika miaka zaidi ya kumi aliyokaa Tanzania.

Mzungu ameyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachorushwa kupitia +255 Global Radio kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kwenye ofisi zake zilizoko kwenye jengo la Global Group Sinza-Mori jijini Dar. 

Pia amewaomba wasanii wenzake kutokuwa wavivu kwenye kazi zao na wawe wabunifu kutoa kazi zilizo bora kukuza muziki wa Kitanzania.

Mzungu Kichaa akiwa katika mahojiano.

…Akiwa na watangazaji wa Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa.

Mhariri wa Risasi Mchanganyiko na Risasi Jumamosi, Erick Evarist (kulia), akimkabidhi Mzungu Kichaa gazeti la ‘Uwazi’ Mzungu Kichaa.

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Global Publishers, Saleh Ally (kulia),  akisalimiana na Mzungu Kichaa.

Wakiongea jambo.

Wakiagana. 

 


Loading...

Toa comment