The House of Favourite Newspapers

Nabii Bendera: Hutaki Chanjo, Unataka Ushirikina? Rais Alichanja Maji? – Video

0

 

ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Ufunuo nchini, Nabii Paul Bendera amewataka watu wanaopotosha kuhusu chanjo ya corona kuacha mara moja ili wale wanaotaka kuchanja wachanje na wasiotaka waache kwani chanjo ni hiari kama ilivyoelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

Askofu Bendera amesema hayo katika kipindi maalum alichofanya Kanisani kwake, Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa maandiko matakatifu yanamtaka kila mtu kuheshimu maamuzi ya mamlaka kwani mamlaka zote zimetoka kwa Mungu.

 

“Kama wakuu wa mihimili yote ya Serikali kuanzia Mhe. Rais amechanja, Makamu wa Rais amechanja, Waziri Mkuu amechanja, Spika wa Bunge amechanja, Jaji Mkuu amechanja, wewe unakuja kutuambia chanjo hiyo haijathibitishwa inamaana  Mhe. Rais alichanja maji? Wewe upo mhimili gani kama unaipinga mihimili ya Serikali?

 

“Kuanzia Israel ambako ndiko Ukristo umeanzia wamechanja, Uingereza ambako ni chimbuko la Dhehebu la Anglican wamechanja, Roma Italy ambako ni chimuko la Roman Catholic wamechanja, Ujerumani ambako ni chimbuko la KKKT wamechanja, Mecca ambako ndiko ulikoanzia Uislam wamechanja tena huwezi kwenda kuhiji bila kuchanja, Sweeden wamechanja, Marekani, Ufaransa, hata jirani hapa Uganda na Kenya wamechanja, wewe ni nani unapotosha?

 

“Kwa sababu chanjo ni hiari waache watu waamue wenyewe, usiwapotoshe, tusimdharau Rais ni taasisi kubwa sio mtu wa kuchezewa chezewa wala kutukanwa. Sio kila jambo lazima uongee mengine unakaa kimya tu. Kama huamini chanjo unataka kuamini ushirikina? alihoji Bendera.

 

Aidha, Askofu Bendera amewataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu janga la corona kwa kujikinga na kufuata taratibu zilizotolewa na wataalam wa afya ikiwemo kuvaa barakoa, kukaa umbali wa mita moja kutoka mtu na mtu, kuepuka misongamano, kunawa kwa vitakasa mikono na mengine.

 

Leave A Reply