The House of Favourite Newspapers

NABII ELISHA, OLIVIA WASIMIKWA RASMI UTUMISHI WA MUNGU

Askofu Dtk. John  Mwakilema (kulia) wa Kanisa la The Word of Prophecy Ministry lililopo mkoani Pwani akiwapaka mafuta ya upako, Elisha na Olivia, kama ishara ya kuwasimika kuwa manabii rasmi.
Manabii wawili wa Kanisa la Repohim lililopo Sinza-Meeda jijini Dar es Salaam, Elisha na Olivia (waliopo chini) wakipata upako kutoka kwa Askofu Mwakilema.
Olivia na Elisha wakipata upako.

MANABII wawili wa Kanisa la Repohim lililopo Sinza-Meeda jijini Dar es Salaam wamesimikwa rasmi kuwa manabii halali baada ya kupakwa mafuta ya upako kutoka kwa Askofu Dtk. John Mwakilema wa Kanisa la The Word of Prophecy Ministry lililopo mkoani Pwani ambapo watakuwa wakiwapa upako watumishi.

Askofu huyo akizungumza wakati wa hafla hiyo amewapongeza manabii hao kwa kufikia hatua hiyo rasmi na kuwataka kutenda vyema kwa watumishi wao katika kuwapa neno la kiroho na kuwapa mafuta ya upako.

Nabii Elisha na mkewe  Olivia wakishikilia vyeti walivyotunukiwa wakati wakisimikwa kuwa manabii rasmi. Katikati ni Askofu Dkt.  John Mwakilema akiwa katika picha ya pamoja. 

Kwa upande wake Nabii Elisha na mkewe Olivia wameahidi kuwalisha watumishi wa Bwana Neno la Mungu ili watumishi hao waweze kurithi ufalme wa Bwana.

Aliongeza kuwa unyenyekevu ndiyo silaha pekee katika maisha ya mwanadamu na leo ndiyo sababu ameweza kupakwa upako kutoka kwa Askofu Mwakilema ili aweze kuwa nabii halali na watumishi wake waweze kulishwa vyema chakula cha kiroho.

Comments are closed.