The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Biteko Awalipua Tanesco Makao Makuu – ”Idara Ya Manunuzi Wawabadilishe” – Video

0


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JHNPP) umefikia asilimia 99 na kwamba mtambo mmoja wenye uwezo wa kufua megawati 235 utaanza kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa mwezi huu na megawati nyingine 235 zitaingia mwezi Machi mwaka huu.

Dk. Doto Biteko ameeleza kuwa vijiji vyote 108 vya Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe vimekwishafikishiwa nishati ya umeme kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Aidha, amesema kuwa katika Wilaya hiyo peke yake, Serikali imetumia shilingi bilioni 9.5 kupeleka umeme.

“Tunapeleka umeme katika vitongoji vyote vilivyobaki, ili watu wote wapate umeme,” ameongeza Dkt. Biteko wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikwavila wilayani humo, mapema leo, Februari 21, katika hafla ya kuwasha umeme katika Shule ya Msingi Ikwavila.

Naye Mbunge wa Wanging’ombe ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Festo Dugange, amekiri na kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati na REA kwa kuvifikishia umeme vijiji vyote 108 vya Wilaya hiyo.

“Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, kati ya vitongoji 525 tulivyonavyo, watendaji wako wachapakazi tayari wametuletea umeme katika vitongoji 295,” amesema.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Godfrey Chibulunje ameeleza kuwa kwa Mkoa wa Njombe jumla ya vijiji 361 kati ya 381 vimekwishafikishiwa umeme wa REA, sawa na asilimia 94.75.

Aidha, vitongoji 1,148 kati ya 1,836 sawa na asilimia 62.5 tayari vimefikiwa na umeme kupitia miradi mbalimbali ya REA.

Leave A Reply