The House of Favourite Newspapers

Nandy Adatisha Uzinduzi wa Guinness Smooth Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

0
Nandy akiwadatisha mashabiki wa burudani kwenye uzinduzi huo.

 

 

 

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Faustina Mfinanga maarufu Nandy ambaye pia ni balozi wa bia ya Guinness Smooth, alikuwa kivutio kikubwa kwa wanafunzi wa vyuo mkoani Mbeya ambao walihudhuria uzinduzi wa bia mpya aina ya Guinness Smooth uliofanyika jana Jumapili.

Baadhi ya washindi wa kuimba na kucheza wakiwa wamekabidhiwa zawadi zao katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti.

 

 

 

Nandy alifanikiwa kuteka mioyo ya wanafunzi waliojitikeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Guinness Smooth ambao walionekana kuwa na kiu kubwa ya burudani ambayo alifanikiwa kuikata.

 

Akiongea katika tukio hilo la uzinduzi, meneja chapa wa SBL, Ester Raphael alisema baada ya uzinduzi wa Guinness Smooth bia hiyo sasa itapatikana kwa wingi katika eneo lote la Kanda ya Nyanda za Juu kusini kwa shilingi 1,500 tu.

Leave A Reply