Nandy Amfungukia Calisa

                                                            Msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’

 Na Mayasa Mariwata| IJUMAA | Story Mix

BAADA ya picha kunaswa zikimuonesha msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ akiwa katika mapozi ya kimahaba na modo anayefahamika kwa jina la Calisa, msanii huyo ameibuka na kufunguka kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi zaidi ya kazi tu.

Akichonga na Stori Mix baada ya picha hiyo kunaswa, Nandy alisema, wengi wanaongea tu wasiyoyafahamu lakini hakuna ukweli wowote kwamba modo huyo ni wa ubani wake. “Ukweli ni kwamba sina mazoea na Calisa kihiivyo, ni mtu ambaye naheshimiana naye wala sijafi kiria kuwa naye kimapenzi, ilikuwa wakati tunaandaa video ya wimbo wangu ndo tulipiga hiyo picha siyo kwamba tulikuwa kwenye mambo yetu binafsi no!” Alisema.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment