Nandy Bye Bye!

BAADA ya kufanikiwa kutinga tatu bora wiki iliyopita, wiki hii haikuwa poa kwa staa wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ ambaye wiki hii mashabiki wa kinyang’anyiro hiki wamemwambia bye bye!

Baada ya Nandy kutupwa nje, sasa wamebaki warembo wawili ambapo ni mshikemshike nguo kuchanika.

Katika shindano hili, warembo 20 walipitishwa na mashabiki wao na wamekuwa wakipigiwa kura za kutoka katika kumtafuta Mrembo Mwenye Mvuto wa Gazeti la IJUMAA (Ijumaa Sexiest Girl 2019/20) ambapo kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa.

Mratibu wa shindano hili ambaye ni Mhariri wa Gazeti la IJUMAA, Sifael Paul amesema baada ya kubaki warembo watatu, ushindani umekuwa ni mkali mno.

Sasa waliobaki kwenye kinyang’anyiro hiki ni Poshy Queen (13) na Mimi Mars (14).

“Unachotakiwa kufanya ni kupiga kura ya nani atoke kwa kuandika jina au namba yake ya ushiriki kisha unatuma kwenda WhatsApp namba; 0713 750 910,” alisema Sifael na kuongeza; “Wadhamini wanakaribishwa kudhamini kinyang’aro hiki kwa kuwasiliana na namba hiyo hapo juu.”

IJUMAA SHOWBIZ

Toa comment