Nandy Kaja Kivingine Wakati wa Corona!

SEXY lady anayekimbiza kunako Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amekuja kivingine kwa kujiingiza kwenye biashara ya kuuza nyama kwa kuwapelekea wateja wake majumbani, hasa wakati huu wa kusambaa kwa Virusi vya Corona.

 

Nandy ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, ameamua kubuni biashara hiyo kwa sababu anaamini itafanya vizuri kutokana na watu wengi, hasa wanaoishi ushuani kutotoka mara kwa mara kwenda buchani, supamaketi au sokoni, wakihofia msongamano wa watu kipindi hiki cha Corona.

 

“Siyo kama nimefulia, ila kwenye maisha unapaswa kujua kusoma alama za nyakati na fursa zilizopo,” amesema Nandy aliyeanzisha Kampuni ya Nandy Meat, Fresh and Healthy inayojishughulisha na usambazaji wa nyama na vitu vingine kama nyanya, vitunguu n.k.

 

Mbali na projekti hiyo mpya, pia anamiliki Kampuni ya Nandy Products inayojishughulisha na usambazaji wa vipodozi Bongo.


Toa comment