The House of Favourite Newspapers

Nape Azifungia Radio 5 na Magic FM Kwa Uchochezi

0

1.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape  Moses Nnauye akitoa taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, ametangaza kuvifungia vituo vya Radio 5 Arusha na Magic Fm Dar kwa muda usiojulikana kwa kosa la uchochezi.

2.Nape akiendelea kusoma taarifa yake.Waziri Nape amesema ameielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuvisikiliza kwa kina kisha kumshauri juu ya hatua zaidi za kuchukua.

3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Aliongeza kuwa kimsingi radio zote mbili kwa pamoja zimetangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake.

4.Waziri Nape akisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari.“Sisi kama Serikali tunatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani, umoja, mshikamano kwa kuwa ni muhimu sana. Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo Agosti 29, 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake” Amesema Waziri Nape.Nape 1

Nape 2

Leave A Reply