The House of Favourite Newspapers

NAY WA MITEGO AMUUMBUA DULA MAKABILA!

0

RAHA ya mahusiano uhakikishe kuwa mwenzi wako anapata amani! Hayo ni maneno ya mwanamuziki wa miondoko ya singeli, Dula Makabila, ambaye yu mahabani na muigizaji, Husna Sajent. Makabila alitoa ushauri huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kumpost Husna na kumuandikia tungo tamu za mapenzi.

Baada tu ya kupost picha hiyo mwanamuziki Nay wa Mitego, akamvaa na kumwambia kuwa maneno hayo ni ya Husna amejiandikia mwenyewe.

Penzi la Makabila na Husna, liliibuka mara baada ya mfalme huyo wa singeli kuachia kibao chake cha ‘Utatoa Hutoi’ ambapo kwa sasa wanaonekana wameshibana sana, na iliwahi kudaiwa kuwa Makabila amempachika ‘kibendi’ mpenzi wake huyo, ila ishu hiyo hawakuwahi kuithibitisha.

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Leave A Reply