The House of Favourite Newspapers

Mwanza: Wanane Wafariki Baada ya Hiace Kutumbukia Ziwa Victoria – Video

0
Taharuki ikitanda baada ya tukio hilo.

WATU nane wamekufa na wawili wameokolewa wakiwa salama baada ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi.

 

“Kwa sasa uokoaji unaendelea, abiria wawili ndio wametoka salama. Maiti nane zimeopolewa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama.

Temesa ndiyo inasimamia kivuko hicho.

 

Hiace iliyotumbukia ziwani.

 

Mshama akizungumzIa ajali hiyo leo Jumatatu amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.

Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.

 

“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.

Updates:

Idadi ya watu waliokufa baada ya Toyota Hiace kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 12.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi  amesema katika ajali hiyo watu watatu wameokolewa wakiwa hai.

 12 Wafariki Baada ya Hiace Kutumbukia Ziwa Victoria – Mwanza

 

Msangi amesema walionusurika wameokolewa na wananchi ambao ni wataalamu wa kuogelea.

Rais Magufuli Waapisha Mawaziri Wapya, Awapa Mwongozo

Leave A Reply