The House of Favourite Newspapers

NCBA Bank Tanzania Yaja Na Kampeni Ya “Maisha Ni Hesabu’ Inayolenga Kuleta Mapinduzi Kwenye Huduma Za Kibenki

0
Ndg. Claver Serumaga, Mkurugenzi Mtendaji wa NCBA Bank Tanzania.

Dar Es Salaam, 20 Septemba — NCBA Bank Tanzania, taasisi kinara kabisa ya fedha nchini, inajivunia kuzindua kampeni yake kubwa kabisa ya, “Maisha ni Hesabu”. Kampeni hii inarasmisha ukuaji wa benki na kuonyesha mbinu zenye tija zinazolenga kuleta mapinduzi katika huduma za kibenki hasa kwa makampuni.

Katika hotuba yake, Ndg. Claver Serumaga, Mkurugenzi Mtendaji wa NCBA Bank Tanzania, alidhihirisha msisimko na matarajio yake na kusisitiza umuhimu wa kuwa na safari yenye mabadiliko.

Alisema, “Leo tunaingia katika safari yenye mabadiliko, tukiongozwa katika misingi ya “Maisha ni Hesabu”. Kampeni hii inalenga kuwajulisha Watanzania kwamba NCBA Bank ipo tayari kuhakikisha wanayafikia malengo yao.

NCBA Bank inaamini kwamba kila siku mfanyabiashara anafikiria kuhusu mahesabu yake, kama kuongeza vitendea kazi vyake, bidhaa zake, kuvuka mipaka na kutanua biashara yake. Hayo yote ni kufikia malengo yake Hivyo NCBA inaamini malengo yake ni mahesabu yake na sisi ni taasisi ya fedha inayohakikisha Hesabu zako zinatimizwa.

Ujumbe mkuu wa kampeni hii unaelezea kwamba namba ama hesabu zina maana kubwa sana katika ulimwengu wa kibiashara.

Kila namba, kila tarakimu ina mchango wake katika mafanikio ya mbeleni. Ndg. Serumaga alikazia, “Tunafahamu kwamba namba zako ni zaidi ya tarakimu; ni uti wa mgongo katika utendaji wako, mapigo ya moyo katika biashara yako.

Na hii ndiyo sababu tumejiandaa vilivyo kuhakikisha unafikia mafanikio, ambayo ndiyo nguzo ya malengo yako ya kifedha.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa, Godson Biyengo, akizungumza na vyombo vya habari baada ya uzinduzi huo.

Kujikita kwa NCBA Bank Tanzania katika kufanikisha malengo yako ya kifedha kunawezeshwa na uwepo wake katika uwekezaji wa rasilimali, imani, uadilifu na ubunifu.

Kama anavyosema Ndg. Serumaga, “Sisi sio benki tu, ni mshirika wako wa kimaendeleo katika kila hali”.

Zaidi ya hapo, benki imejikita katika kuleta maendeleo ya kidigitali kwa kuwekeza zaidi kutengeneza mfumo mpya wa kidijitali (Mobile Banking) unaowezesha wateja wetu kufanya miamala muda wowote na popote walipo.

Kampeni ya “Maisha ni Hesabu” inahamasisha wafanyabiashara kuwa na fikra mpya kwenye mfumo wao wa kifedha na kuangalia ni jinsi gani namba zina nguvu za kupeleka biashara zao mbali zaidi. Wakiwa na NCBA Bank Tanzania, wafanyabiashara hawatakuwa tu na taasisi ya kifedha, bali mshirika sahihi, mwenye Mawazo ya mbali aliyejikita katika kuendeleza na kutimiza ndoto zao za kiuchumi.

Huu ndio muda sahihi wa kufikiria namba katika namna nyingine, na mshirika sahihi ambae ni NCBA Bank. Jiunge sasa na NCBA Bank Tanzania na tuandike historia itakayokuja kuleta tija kwa vizazi vijavyo.

Leave A Reply