The House of Favourite Newspapers

Ndayiragije apania rekodi Azam FC

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije, amesema, anachokifanya kwenye michuano ya Kagame nchini Rwanda ni kusaka rekodi ikiwemo kutetea kombe lao hilo.

 

Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambayo mwaka huu inafanyika Rwanda, Jumapili iliyopita ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Idd Seleman ‘Nado’ dhidi ya Mukure FC ambapo jana walishuka dimbani kuvaana na KCCA ya Uganda.

 

Ndayiragije raia wa Burundi, huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC baada ya kujiunga nayo akitokea KMC. Akizungumza na Championi Jumatano, Ndayiragije amesema anataka aweke rekodi akiwa na Azam FC ya kuchukua Kombe la Kagame kwa mara ya tatu ili ajitengenezee njia ya kuelekea kulitwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu ujao.

 

“Kila kocha anahitaji rekodi kwenye kila timu, hivyo mimi nataka niiwezeshe Azam FC kutwaa Kombe la Kagame kwa mara ya tatu mfululizo, ambapo naamini hiyo itanipa nguvu ya kuliwania Kombe la Ligi Kuu Bara msimu ujao,” alisema Ndayiragije.

Comments are closed.