The House of Favourite Newspapers

Ndege ya Tanzania Air-Bus A220 Yatua Accra, Kutua Kesho

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini.

Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege.

Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220.

 

“Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona Twiga na jina la nchi yetu Tanzania ambalo lina sifa kubwa duniani” amesema Balozi Mboweto.

Balozi amesema Watanzania waishio Nigeria na Ghana wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano na Mhe. Rais Magufuli kwa mafanikio haya makubwa ambayo yatasaidia kukuza uchumi kupitia usafiri wa anga, utalii na uwekezaji.

 

Ndege hiyo A220 iliondoka Montreal Canada jana saa 1:00 Jioni kwa saa za Canada na ikatua visiwa vya Santa Maria saa 5:00 usiku kwa saa za huko.

 

Hii leo imetua Accra Ghana majira ya saa 4:00 kwa saa za Ghana na kupokelewa na Balozi Muhidin Mboweto wa Nigeria anayehudumia na Ghana.

 

Pamoja na marubani wa kampuni ya Air-Bus na Marubani wa Tanzania walioongoza katika safari ya ndege hiyo kuja nchini Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi ndiye anaongoza safari ya ndege hiyo kutoka Canada hadi itakapowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kesho Itatua saa 8:30 mchana.

Accra, Ghana.

Comments are closed.