The House of Favourite Newspapers

Ndege Yaanguka Barabarani na Kuuwa Watu Sita Mji Mkuu wa Haiti, Port-au-Prince

0

Ndege ndogo imeanguka kwenye barabara kuu katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince na kusababisha vifo vya takriban watu sita.

Ndege hiyo ilikuwa njiani kutoka mji mkuu kuelekea mji wa bandari wa kusini-mashariki wa Jacmel ilipoanguka katika kitongoji cha Carrefour.

 

Ilijeruhi watu kadhaa wa chini. Rubani alikuwa mmoja wa wale ambao awali walinusurika lakini alikufa kutokana na majeraha yake hospitalini baadaye.

Maafisa walisema kufeli kwa injini ndio tatizo. Ndege hiyo ilikuwa imetuma ishara ya itilafu dakika 20 baada ya kupaa, mamlaka ya usafiri wa anga nchini ilisema.

 

Waziri Mkuu Ariel Henry alielezea huruma na “familia za wahanga, ambao wameingia kwenye ukiwa mkubwa zaidi na mkasa huu mpya”.

Nchi hiyo masikini imekumbwa na majanga kadhaa ya asili katika miaka ya hivi karibuni ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na uchumi.

Vurugu za magenge hayo pia zimezidi kuwa mbaya kutokana na mzozo wa kisiasa kufuatia mauaji ya Rais Jovenel Moïse Julai mwaka jana.

SIMBA Wafanya UMAFIA, WATUA Afrika Kusini MAPEMA, YANGA Wamnasa STRAIKA Hatari | KROSI DONGO

Leave A Reply