The House of Favourite Newspapers

Ndege Yaanguka Serengeti, Watalii, Rubani Wajeruhiwa

0
Ndege hiyo baada ya kuanguka.

NDEGE  iliyoikuwa imebeba watalii kumi na rubani mmoja jana Jumatano, Oktoba 25,2017 ilianguka kujeruhi watalii wawili na rubani wakati ikitua katika uwanja wa Lobo ulio katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Kuanguka kwa ndege hiyo ya Kampuni ya Coastal Aviation imethibitishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema ambaye amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana majira ya saa tisa alasiri ilipokuwa ikijaribu kutua.

Mwakilema amesema chanzo cha ajali hiyo ni mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kusababisha uwanja kujaa maji na akaongeza kuwa wakati rubani akitua  ndege ilianguka na kusababisha watalii hao wawili kujeruhiwa.

Ilivyogonga mti.

“Ni kweli ajali ilitokea jana, majeruhi ni wawili na rubani, walipelekwa Arusha na baadaye kusafirishwa Nairobi kwa matibabu zaidi. Wengine walikuwa na maumivu kidogo, walipatiwa huduma na daktari wetu na kisha wakasafirishwa kwenda Arusha,” alisema Mwakilema.

“Tunamshukuru Mungu kwa kweli, maana hata ndege haikuungua, ilipokuwa ikiserereka iligonga mti na kusimama. Mbele palikuwa na mawe, hivyo ingeyagonga na kulipuka ingesababisha madhara makubwa zaidi,” aliongeza Mwakilema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu ameeleza kusikitishwa kwake na ajali hiyo huku akisema wanaendelea kufuatilia chanzo chake na kwamba, wanasubiri taarifa kutoka kwa vyombo husika vinavyochunguza ajali hiyo.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

==

VIDEO: Lulu Alimuua Kanumba Bila Kukusudia – Wazee wa Baraza

Leave A Reply