The House of Favourite Newspapers

Ndoa na Shetani-10

1

ILIPOISHIA:
“Wewe ni mwanamke gani kama msala wa kituo cha basi kila abiria anajisaidia halafu unajiita mzuri tena unayajua mapenzi. Kwa uzuri kweli mzuri hakuna kati yetu anayekufikia pia tuna imani mapenzi unayajua lakini ulitakiwa kumfanyia mume wako si mume wetu.

Hivi tukiachika na uzee huu twende wapi, unajua ndoa zetu zimedumu miaka mingapi halafu wewe shetani wa kike utuharibie?” alisema mama mmoja mtu mzima aliyekuwa amefunga mtandio kiunoni.
SASA ENDELEA…

“Najua nimefanya makosa, mimi ni kama mtoto wenu naomba mnisamehe,” nilijitetea kwa vile ilionekana wananijua vizuri baada ya kunifuatilia kwa muda mrefu.
“Wee… weee, tena koma kusema tukusamehe eti mtoto wetu wakati mwanamke mwenzetu mwenye uwezo wa kutembea na wanaume wa dunia nzima,” alisema mama mmoja ambaye nywele zake zilikuwa timtim kuonesha walimkurupua na kuja bila kujiandaa.”

“Yaani ana bahati sijui bila kunikataza leo naona tungegawana majengo yeye mochwari na mimi gerezani,” mwanamke mwingine aliyekuwa pekupeku alisema kwa hasira bila kujua alipanga kunifanya nini japo ilionesha alidhamiria kuniua.

“Jamani pamoja na yote waume zenu sikuwafuata ila wao ndiyo walinifuata, kwa vile nimejua kosa langu nakuahidini kuachana nao. Chondechonde nipo chini ya miguu yenu msinifanye kitu kibaya,” nilijitahidi kuwabembeleza ili waniachie.

“Kwa vile ulikosesha amani ya nyumba nyingi na kuwa na wasiwasi wa kuvunjika kwa ndoa zetu, kama nyumba zilizotiliwa alama ya X ambayo ingebomolewa wakati wowote. Tumekuandalia zawadi nzuuuuri ambayo itabakia kumbukumbu katika maisha yako.

“Baada ya zawadi hiyo utakuwa na hiyari ya kuendelea na tabia yako au kuachana nayo kabisa. Unawaona vijana hawa walioshiba, tuna imani watamaliza hamu zako zote na kukufanya uachane na waume zetu….vijana kazi kwenu.”

Nilichanganyikiwa kwa kujua vidume vile sita vitaniingilia kwa pamoja niliona kama maisha yangu yatakuwa rehani. Nilijitahidi kuomba radhi huku nikilia kwa kuwaahidi sitarudia tena lakini ilikuwa kazi bure.

Baada ya kusema vile waliondoka na kuniacha na kundi la wanaume zaidi ya sita ambao bila kuchelewa walinivamia na kunivua nguo zote na kubakia mtupu na kulazwa kitandani kisha nilifungwa kamba miguu na mikono kama nasulubiwa na kuanza kunibaka kwa zamu huku nikihisi maumivu makali kwa vile hawakufanya jambo lile kistaarabu.

Baada ya kumaliza kunibaka nikiwa kwenye hali mbaya hawakuniacha vilevile walinishushia kipigo kitakatifu ambacho kilinifanya nipoteze fahamu. Nilizinduka siku ya tatu na kujikuta nipo hospitali nikiwa nimefungwa bandeji baadhi ya sehemu za mwili wangu, nilikuwa hoi, ulikuwa unauma kama kidonda.
Baada ya muda nilirudisha kumbukumbu, roho iliniuma sana na kuanza kulia kilio cha chinichini huku nikijutia yote yaliyonikuta na kuamini ile ni radhi ya wazazi wangu kwa kukimbia nyumbani bila ridhaa yao. Moyo uliniuma sana kwa kitendo cha kinyama walichonifanyia.

Bado niliamini matukio yote yaliyonikuta ilikuwa ni laana ya wazazi wangu, niliamini kabisa kipindi kile nilitakiwa kurudi kwa wazazi ili kuomba msamaha kwani niliamini mwisho wangu ungekuwa mbaya sana. Nilikaa hospitali mwezi mmoja na nusu, baada ya kupata nafuu niliruhusiwa kurudi nyumbani.

Nilipofika nyumbani nilikuta pigo jingine baadhi ya vitu vyangu na pesa vilikuwa vimeibwa. Nakumbuka siku niliyotekwa mlango wa chumbani sikuufunga. Ilionesha mlinzi baada ya kujua nipo kwenye hali gani aliam
Itaendelea katika Gazeti la Risasi Jumamosi.

1 Comment
  1. Prince'otto says

    pole sana ant konso

Leave A Reply