The House of Favourite Newspapers

Ndoa na Shetani – 28

0

ILIPOISHIA:
“Kama nilivyokueleza kazi yangu ina sura mbili,  kuna kitu tunataka kukifanya ili kuwaziba watu macho hata ukiwa msaidizi wangu basi watu wawe na ushuhuda wa kweli.”
“Sawa, nieleze hiyo kazi.”
“Kanisa langu limepata sifa nyingi kutenda miujiza ambayo mingi huwa ya kutengeneza kama huu nitakao utengeneza kwako.”
“Huo muujiza upi?”
SASA ENDELEA…

Sasa hivi matajiri wamekuwa wabahili, sadaka zako zimepungua, baada ya kukaa kwa muda tumebuni njia mpya ambayo tutatumia kuzipata pesa zao bila wao kujua.”
“Kuzipata kivipi?”
“Kuna njia ya wao kuleta pesa zao bila kujua.”
“Sasa hiyo si chuma ulete.”
“Sawasawa kabisa.”
“Mmh! Tunafanyaje?”
“Kwa vile wewe ni mgeni  tunataka tukupe ugonjwa wa wenda wazimu huku damu za siku zako zikitoka mfululizo.”
“He! Halafu?” nilishtuka na kutaka kujua mwisho wake.
“Baada ya zoezi hilo nakulipa pesa yako kisha tunaanza biashara nyingine.”
“Sasa nikiugua wendawazimu na kutokwa na damu nisipopona nini hatima yangu?” woga uliniingia japokuwa pesa naitaka.
“Konsooo, huugui bali utaigiza kama mwendawazimu ambaye utaonekana kwenye majalala kwenye soko na maeneo ya kanisani kwa muda wa wiki mbili baada ya hapo tutamalizia zoezi lile na wewe kukutoa pepo kanisani kwangu na baadaye utatoa ushuhuda mbele ya hadhira huku watu wakiamini kuwa ni ushuhuda wa kweli kwa vile watakuwa waliwahi kukuona ukiwa chizi hapo nitaongeza waumini hata sadaka itaongezeka.”
“Mmh! Usiku si naweza kubakwa?” niliingia wasiwasi wa kulala kwangu  kwa kuhofia kubakwa kwa vile ningekuwa nikilala kwenye majumba mabovu au sokoni.
“Hakuna anayeweza kukugusa hata polisi hawatakusumbua, utakuwa salama muda wote.”
“Usiku nitalala wapi?”
“Kazi yako utaianza saa kumi na nusu alfajiri na kumaliza saa mbili usiku, muda wote utakuwa na mtu anakulinda, kwa umbile lako lazima kuna wakora watakupigia hesabu za usiku wakubake.”
“Usiku nitaondokaje?”
“Kuna gari litakufuata na kukurudisha nyumbani utaoga, utakula na kupumzika kujiandaa kwa ajili ya kazi ya siku inayofuata.”
“Mmh! Sawa.”

“Wewe ifanye kazi yako vizuri utaona kitakachofuata, nakuapia utakuwa kiumbe mwingine mwenye jina kubwa ndani na nje ya nchi katika kufanya miujiza.”
“Suala la kufanya vizuri hilo ondoa shaka umeleta sanaa ndani ya jumba la sanaa,” kazi aliyonipa wala haikunipa shida, hata ingekuwa nyumbani Tanzania ningefanya chochote ambacho ningeelekezwa kwa vile baada ya kazi napewa changu nakuwa kama naigiza filamu.
“Hutaona aibu?”
“Nisimuonee aibu ninaye mvulia nguo ya ndani bila kumjua itakuwa kuigiza nina kichaa, hiyo kazi nyepesi,” nilimtoa shaka.
“Itabidi ufanye mazoezi kabla ya kuanza kazi.”
“Sihitaji zoezi niliisha wahi kuigiza shuleni, hilo ondoa shaka, kwa vile mimi mgeni wa jiji hili  nitembezeni kwenye gari ili nijue nitapita wapi na wapi  ili nisipotee.”
“Hakuna tatizo, inaonekana unajiamini sana.”
“Ninaposikia pesa akili yangu huwa haihofii kitu chochote, kwangu mimi nitakuwa kama nipo location nikiigiza filamu isiyo na mtu wa video kamera.”

“Unazidi kunipa matumaini ya kuifanya kazi vizuri.”
“Hilo shaka ondoa, vipi kuhusu rafiki zangu, japo umesema siri ibakie kwetu. Watanielewaje wakiniona nimechizika? Lazima watataka kunipa msaada na kuharibu mpango wetu.”
“Tena wao ndiyo watatusaidia kufanikisha mpango wetu ndiyo watakaokukamata na kukuleta kanisani kufanyiwa maombi nao pia watapata malipo mazuri.”
“Mmh! Kama hivyo sawa, kwa hiyo baada ya kazi hiyo wataendelea na kazi yao?”
“Hapana watakuwa wapambe wako katika kazi zako zote, kupitia wewe nao maisha yao yatabadilika.”
“Hilo litakuwa jambo zuri,” nilifurahi rafiki zangu nao kupata dili.
“Kesho nitaonana nao ili niwaelekeze cha kufanya.”
“Hapo nimekuelewa, sasa nitaifanya kazi yako moyo wangu ukiwa baridiii.”
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, tulimalizia raha zetu na kupumzika kuitafuta siku ya pili.
***
Siku ya pili niliwafuata kina Doi ili niwapeleke kwa Papaa, niliamini kupitia mimi ile ndoto ya kuacha kupigwa na baridi na kuumwa na mbu itatimia. Siku hiyo niliwafuata mwenyewe na gari la kifahari aina ya BMW.
Usikose mwendelezo wake katika gazeti la risasi jumamosi.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply