The House of Favourite Newspapers

Ndoa Ya Diva Na Sheikh Abdulrazak Chali, Mwenyewe Afunguka – “Single Lady”

0

Habari iliyozua mshtuko kwenye ulimwengu wa mastaa wa Bongo usiku wa kuamkia leo Januari 13, 2023 ni kuhusu sintofahamu ya ndoa ya mtangazaji wa Wasafi, Diva The Bawse na mumewe, Sheikh Abdulrazak Salum kwamba ni chali.
Diva ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo single; yaani hana mwanaume au hayupo kwenye uhusiano na kimapenzi na mwanaume yeyote.Jambo hilo limezua mjadala mzito kutokana na namna ambavyo wawili hao wamekuwa waklioneshana mapenzi shatashata tangu walipofunga ndoa iliyojaa matashtiti yapata mwaka mmoja uliopita.
Kupitia ukurasa wake wake wa Instagram, Diva amefunguka kuwa ni rasmi yeye ni “SINGLE LADY”
Pamoja na mshtuko wa wengi, lakini inaonekana wazi kwamba Diva na Sheikh Abdulrazak hawapo pamoja kwa sasa na huwenda ndoa yao imevunjika!

STORI NA SIFAEL PAUL, GPL

Leave A Reply