The House of Favourite Newspapers

Ndugai Awataka Wabunge Kurejea Dodoma-Video

0

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amewataka mawaziri, wabunge wote waliopo nje ya Jiji la Dodoma kuacha shughuli wanazofanya na kurejea haraka Dodoma, kuhakikisha kesho Aprili 22, wanakuwapo bungeni kumsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema hotuba itakayotolewa kesho na Rais Samia ni muhimu kwa wabunge wote na Watanzania, hivyo ni lazima kila waziri, mbunge kuwamo bungeni.

Kwenye taarifa yake Spika Ndugai amesema: “Naomba nisisitize kwamba kesho kila mtu lazima awepo bungeni. naomba wabunge muwaambie wenzenu ambao hawapo Dodoma.

 

Hata mawaziri waache shughuli zao warejee bungeni, itakuwa jambo la aibu wageni kujaa kila sehemu ya bunge halafu ndani ya Bunge kuna ma-gap ( nafasi) wabunge hawapo”.

 

Leave A Reply