The House of Favourite Newspapers

Ndugai: Marekani Wanamshughulikia Trump, Tumshugulikie Zitto – Video

0

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema kama Bunge la Marekani linamshughulikia Rais wa nchi hiyo, Donald Trump,  kwa vitendo vya kukosa uzalendo, kwa nini isiwe kwa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ambaye amefanya kitendo cha kuisaliti  nchi?

 

Amesema hayo jana Ijumaa Januari 31, 2020, bungeni mjini Dodoma wakati akihitimisha hoja iliyoletwa na  Mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel.

 

Mollel  amewasilisha hoja binafsi bungeni akiwashauri wabunge wamuunge mkono kufikia uamuzi wa kumchukulia hatua Zitto  kwa kitendo chake cha kuandika barua Benki ya Dunia (WB) akitaka Tanzania isipewe mkopo wa Dola 500 milioni za Marekani kwa ajili ya sekta ya elimu.

 

Ndugai amewaambia wabunge kuwa jimboni kwake baadhi ya shule wanafunzi hawana madawati wanakalia vigoda vya miguu mitatu.


 

Pia,  amesema kuna shule ya sekondari ina vyoo viwili, kimoja kinatumiwa na watoto wa kike na kingine kinatumiwa na wavulana.

 

Amongeza kwamba kitendo cha Zitto ni usaliti kwa kuwa fedha hizo zingesaidia kuondoa changamoto nyingi kwenye sekta ya elimu.

 

Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Mkamia, akichangia hoja ya usaliti wa Zitto ametoa mfano wa Wamarekani kwamba rais wake anayesaliti taifa lao hawamuachi salama. Amesema kuna haja Bunge likachukua hatua kwa watu kama Zitto.

 

Leave A Reply