The House of Favourite Newspapers

NEC Yamteua Shibuda Urais ADA-TADEA, Atoa Ujumbe – Video

0

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua John Shibuda kuwa mgombea wa urais wa Tanzania na Hassan Kijogoo kuwa mgombea umakamu rais chama cha ADA-TADEA.

 

Zoezi hilo limefanywa leo Jumanne, Agosti 25, 2020 na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage kwenye ofisi za NEC Dodoma.

 

“Kila chama kina ubora wake, katika masuala ya kisiasa kuna namna ya kutoa ujumbe, kuna vijembe kuna maneno ya kufanya jamii ivutiwe na hisia zako za kisiasa, hakuna chama kafara kwa ajili ya kubeba na kushindisha chama kingine.

“Kila chama kinachoingia kwenye uchaguzi huu kinakwenda kutafuta ushindi, na mimi nitakwenda kupeleka changamoto, kukosoa na  kusahihisha.  Mtu asitegemee kampeni zitakuwa kama mahubiri ya kidini. Tunakuja na maono ya kushindanisha vyama ili wananchi wachague chama wanachokitaka kiwape maendeleo,” amesema Shibuda.

 

Leave A Reply