The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-32

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Nelly alipomfahamisha Ipyana kuhusu yule mama mtu mzima aliyefika eneo walilokuwa wakioshea magari. Je, kilifuatia nini? Songa mbele…

“Huyo mama anaitwa mama Maduu alifiwaga na mumewe kitambo tu na siyo bahili wa fedha zake, kwani kuna wakati nikimuoshea gari lake hunipa mpaka shilingi elfu kumi,” Ipyana alimwambia rafiki yake na kuongeza;
“Halafu mama huyo anapenda sana vijana wadogo,” Ipyana alimwambia Nelly ambaye moyo wake ulipiga paa kwa kupata taarifa hiyo.

Wakati wakiendelea na maongezi yao, kumbe mama Maduu ambaye ofisi yake ipo ghorofani aliwaona akatoka na kushuka kwa lifti na kuelekea kwa akina Ipyana.
“Ipyana hujambo?” alimsabahi.
Baada ya salamu alimwambia kwamba alimuona ndugu yake na kumtania kama alikuja kumfundisha kazi ya kuosha magari,” Ipyana akamwambia alikuwa anajua.
Mama huyo alipopewa jibu hilo alimwambia hakuwa na muda mrefu alitaka wamuoshee gari lake na kwamba atafurahi sana kama kazi hiyo nitaifanya mimi, akaahidi liking’aa atanipa zawadi ya kunikaribisha kisha akawa anaelekea ofisini.
“Da! Ukisikia mtu nyota yake inang’aa bila kwenda kwa mganga ndiyo mimi, yaani hata huyu mama inavyoonekana ananitaka, dalili zote zipo wazi,” Nelson Nzamba a.k.a Nelly aliwaza.

“Kaka si nilikuambia kuhusu wanawake wa hapa, umemsikia alivyokuambia mama?” Ipyana alimwuliza Nelly.
“Kaka sina cha kusema ila ndani ya wiki yule sijui dada Jully, Fatu au huyu mama lazima mmoja nitakupa ripoti kwamba nimeua, wewe subiri kwani  siwezi kuwaacha viumbe wenye hela zao wajishaueshaue wakati fyekeo ninalo.
Ipyana alicheka sana na kumwambia awe makini lakini kwa sababu pale wizarani ngoma ilikuwa njenje, Nelly akamwambia hakuna binadamu atakayeishi milele acha ale ujana.

Siku hiyo waliosha magari na kupata shilingi 46,000 achilia mbali shilingi elfu kumi aliyopewa Nelly na yule mama Maduu aliyejifanya kampa ofa ya kumuoshea gari lake vizuri kumbe alikuwa na lake jambo!
Kufuatia urafiki wao, baada ya kumaliza kazi Nelly na Ipyana walioga na kuvaa pamba zao na kuelekea kituo cha daladala cha Posta Mpya kupanda basi la Tandika.
Wakiwa kituoni Nelly ambaye mfukoni alikuwa na shilingi elfu 20 alimwambia Ipyana kwamba akifika Keko atashuka anataka kwenda kumuona mshkaji wake mmoja, Ipyana aliyemshtukia kwamba yalikuwa ni masuala ya mademu akacheka sana.
“Mbona unacheka?” Nelly alimwuliza.

“Wewe si useme unataka kwenda kuonana na mtoto unafikiri sikufahamu Nelly?” Ipyana akamwambia.
Kama kawaida yake, Nelly alicheka ndipo Ipyana aliyekuwa akipenda sana maendeleo akafungua waleti yake akachomoa wekundu wawili wa msimbazi akampatia Nelly aliyeishia kuporomosha tabasamu kwani alijua ishu yake ya kukutana na Atu itakwenda vizuri.

Wakiwa pale kituoni basi la Tandika lilifika wakapanda na kukaa siti moja, kama unavyojua pande za Posta kulivyo na mademu wazuri, Nelly akawa macho juu kuwaangalia na kula kwa macho maana aliziona shep za kila aina.
Gari lilipoondoka, akapigiwa simu na Doreen aliyemtaka afanye awezavyo kesho yake waonane lakini Nelly alimwambia amsubiri mpaka wikiendi kwani sehemu aliyoanza kazi walikuwa bize sana.
Doreen hakuwa na jinsi zaidi ya kuwa mpole na kumwomba usiku wakutane kwa njia ya meseji ili amkate kiu kwa kutumia usanii wake kama alivyomfanyia siku ile.
“Usijali mpenzi wangu, nitafanya hivyo,” Nelly alimwambia Doreen.
Gari lilipofika Keko, Nelly alimuaga rafiki yake Ipyana na kumwambia wataonana nyumbani, Ipyana akaishia kucheka na kumtakia Nelly kazi njema.

Nelly alipoambiwa hivyo huku akishuka kwenye gari akawa anacheka kwani alijua alichokimaanisha Ipyana, gari lilipoondoka akiwa pembeni ya barabara alimpigia simu Atu.
“Niambie mpenzi wangu umeshafika?” Atu alimwuliza.
“Yeah! Wewe uko wapi?”
Baada ya kuulizwa hivyo, Nelly alimwambia alikuwa kituo cha daladala ndipo Atu akamwambia kwa kuwa eneo lile watu walikuwa wakimfahamu atangulie katika gesti waliyokutana siku ya kwanza.
Itaendelea wiki ijayo, maoni tumia namba hiyo hapo juu.

Leave A Reply