The House of Favourite Newspapers

Newcastle Yanunuliwa na Waarabu

0
Saudi Arabia Public Investment Fund wamekamilisha dili la ununuzi Klabu ya Newcastle United inayoshiriki Ligi Kuu ya England (Premier) kwa asilimia 80 kwa dau la paundi milioni 300 kutoka kwa mmiliki wa zamani ambaye ni Mike Ashley.
Asilimia 20% ya umiliki huo zinatoka PCP na RB Sports & Media ambapo zimekamilisha kupatikana kwa asilimia 100% ya uuzwaji wa klabu hiyo.
Saudi Arabia Public Investment Fund chini ya Mwenyekiti Mohammad Bin Salman ambaye ni Crown Prince Wa Saudi Arabia ambao wamefanikisha hilo baada ya kuanza mchakato huu wa kutaka kuinunua klabu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.
Mashabiki wa Klabu hiyo wanamtaka mmiliki wa zamani, raia wa Uingereza, Mike Ashley ajiuzulu.
Wamiliki hao wapya wa klabu ya Newcastle wanakadiriwa kuwa na utajiri mara 10 zaidi ya utajiri wa mmiliki wa Klabu ya Man City, Sheikh Mansour hivyo tarajia kuiona Newcastle kwenye levo za Man City.
Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply