The House of Favourite Newspapers

Mwanamke Auawa kwa Mapanga

0

Serengeti. Watu watatu ambao hawajajulikana wamemuua Sikujua Maghembe (51) mkazi wa Kitongoji cha Nyakitono Kijiji cha Makundusi Kata ya Natta Wilaya ya Serengeti kwa kumkata koromeo na kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Longinus Tibishibwamu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo Oktoba 6 majira ya kati ya saa 1.30 usiku nyumbani kwa mwanamke huyo na watuhumiwa hawakuchukua kitu.

“Baada ya kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo chake walikimbia bila kuchukua kitu,tunaendelea na uchunguzi,tunaomba wananchi watupe ushirikiano ili tuweze kuwakamata wahusika,”amesema.

Joseph Nyaikobe Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Makundusi amesema wakati wanaingia nyumbani kwa Sikujua waliwamlika kwa tochi zenye mwanga mkali kisha wakampiga kwa ubapa wa panga Elias aliyekuwa anaishi na mama huyo kama wapenzi baada ya kufiwa na mme mwaka jana.

“Huyo Elias,watoto wawili wa marehemu mmoja aliyekuwa anapika na mwingine mdogo nao wakakimbia wakati watuhumiwa hao wakimshambulia huyo mama,kwa kweli amekatwa sana,kichwani katikati,pembeni,katikati ya paji,mikono na kumkata koromeo,” amesema.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyakitono Nginda Masanyiwa amesema pamoja na jitihada za wananchi waliosikia yowe na kufika eneo la tukio kufuatilia maeneo mbalimbali hawakufanikiwa kuwanasa watuhumiwa.

Amesema mazishi ya mama huyo yanafanyika leo Oktoba 7 nyumbani kwa marehemu baada ya uchunguzi wa kitabibu na polisi kukamilika.

Leave A Reply