The House of Favourite Newspapers

NEYMAR, MBAPPE WAZINGUANA PSG

MASTAA wa Paris St. Germain, Neymar na Kylian Mbappe inasemekana wamekorofishana, habari hii inadaiwa kuwafurahisha Real Madrid. Mbappe na Neymar kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakihusishwa kutaka kuondoka PSG na kutakiwa na Real Madrid.

 

Watu hao inadaiwa wamekuwa hawapikiki tangu timu hiyo ilipofungwa na Rennes kwenye mechi ya Kombe la Ufaransa katika mchezo ambao Mbappe alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

 

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Neymar baada ya kipigo kile alituhumu wachezaji wenzake ndio waliosababisha timu yao kuboronga. Maneno yake inadaiwa hayakumfurahisha Mbappe kutokana na ukweli kuwa alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya mchezo ule, ambao PSG ilifungwa kwa penalti.

 

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Real Madrid kwa sasa inafuatilia kwa karibu taarifa za ugomvi wa Mbappe na Neymar, ikiangalia uwezekano kumpata miongoni mwa mastaa hao. Habari zinaeleza kuwa ugomvi huo ni sababu mojawapo iliyofanya Mbappe kutoa kauli ya kutishia kuondoka katika klabu hiyo.

Comments are closed.