JUZI Jumamosi mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, walikuwa wageni wa Majimaji, timu ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Sokabet, timu hizo zilikutana kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea lakini kuna mambo kadhaa ya kujifunza.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, kuna mambo kadhaa ambayo yalionekana kuwa na maana kubwa katika soka la Majimaji, Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa jumla.
1. FEDHA NI CHACHU YA MAFANIKIO
Hivi karibuni Majimaji ilikimbiwa na Kocha Kally Ongala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kutolipwa haki zake, hiyo ilisababisha hata morali ya wachezaji kushuka, lakini ujio wa Sokabet umeamsha moyo wa upambanaji wa wachezaji na hata viongozi wenyewe wanaonekana kuwa tayari kupambana kwa timu yao.
2. SONGEA WANAPENDA MPIRA
Licha ya ukongwe wa Majimaji katika soka la Tanzania, lakini miaka ya hivi karibuni ilionekana kama tamaduni ya watu kuipenda timu yao ilipungua, lakini ujio wa Sokabet umeongeza chachu ya wadau kujitokeza kwa wingi kuisaidia na kuiunga mkono timu yao hiyo. Juzi wengi walijitokeza uwanjani na hata hamasa kabla na wakati wa mchezo ilikuwa kubwa.
3. WANAWAKE WA RUVUMA NI WANASOKA
Licha ya kuzoeleka kuwa soka ni mchezo unaopendwa na wanaume lakini wanawake nao huwa wapo wenye mapenzi kama wanaume katika tasnia hiyo, upande wa Ruvuma kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki wa kike wasichana na wamama waliojitokeza uwanjani na baadhi yao walikuwa wamevaa jezi za Majimaji mpya zilizo na nembo ya Sokabet, hiyo inathibitisha jinsi ambavyo wanawake wa Songea na Ruvuma kwa jumla walivyo tofauti.
4. TIMU ZA MIKOANI ZINAHITAJI WADHAMINI
Hali ya klabu za Simba, Yanga na Azam FC kupata wadhamini kila kukicha kumezifanya timu hizo kuwa na nguvu uwanjani na hata nje, lakini uwepo wa Sokabet ndani ya Majimaji unathibitisha jinsi uwepo wa wadhamini unavyoweza kusaidia timu za mikoani kwa kuwa tangu kampuni hiyo ianze udhamini mwamko wa upambanaji ndani ya Majimaji umekuwa juu.
5. SOKABET INA NAFASI YA KUJITANUA
Kitendo cha Majimaji kuonekana kuwa na nguvu mkoani kwake kwa watu wake kuiunga mkono kwa kununia jezi zenye nembo ya mdhamini, kunamaanisha kampuni hiyo ikiamua kutanua udhamini wake hata kwenye timu nyingine, inaweza kufanikiwa na itachangia katika kukuza soka la ushindani nchini, ili mwisho wake tupate wawakilisha imara wa kimataifa.
Akizungumzia juu ya mikakati yao, Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda, alisema: “Ni mapema kuelezea mikakati lakini kadiri ambavyo tunaendelea kupata nguvu katika klabu tunayoidhamini, hiyo itatupa nguvu ya kuongeza udhamini kwa Majimaji ama kwingine kwa kuwa kampuni yetu ina mikakati mikubwa na ina nia njema ya kukuza michezo ya Tanzania kwa kuwekeza, siyo katika soka tu.
“Lakini ili kukamilisha hilo, nawaomba washiriki ambao wanaanzia umri wa miaka 18 kuendelea, kujiandikisha zaidi na kushiriki kubashiri matokeo katika tovuti yetu ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani mshiriki anaweza kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kubeti kwa buku tu.”
JOHN JOSEPH, Aliyekuwa Songea.