The House of Favourite Newspapers

NHIF: Hospitali Binafsi Zinazositisha Huduma Zinakiuka Mkataba, Tunasajili Vituo Vipya

0

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema umeona matangazo ya kusitishwa huduma kwa Wanachama wa NHIF kwa baadhi ya vituo binafsi; Regency Medical Center, Kairuki, Hospitali za TMJ, Hospitali ya Apollo na Hospitali zote za Aga Khan Nchini kuanzia leo Machi 1, 2024 na kueleza uamuzi huo ni kinyume na mkataba wa utoaji huduma wa pande mbili

Meneja Uhusiano wa NHIF, Angela Mziray amesema mkataba uliopo unamtaka Mtoa Huduma kutoa notisi ya Siku 90 kabla ya kusitisha huduma

Amesema “Wanachama watumie vituo mbadala, Maafisa wa NHIF watakuwa vituoni kusaidia Wanachama wenye changamoto kupata huduma katika vituo vingine, Mfuko unawasiliana na wenye matibabu yanayohitaji mwendelezo wa huduma ikiwemo huduma za kusafisha damu (dialysis) ili kuwaelekeza vituo mbadala na tunafanya usajili wa vituo vingine binafsi.”

Leave A Reply