The House of Favourite Newspapers

NI HISTORIA: Aston Villa Wamtambulisha Rasmi Samatta

0

 MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta,  baada ya kusubiri kwa muda, hatimaye ametia saini ya kuichezea Aston Villa kwa mkataba wa miaka minne.

Usiku wa kuamkia leo, Januari 21, 2020,  klabu ya Aston Villa kupitia ukurasa wake wa Twitter  na Instagram, wamemtambulisha Samatta.

Nahodha huyo wa Taifa Stars anajiunga na Villa akiwa na kibarua kizito cha kuhakikisha timu hiyo inajiondoa katika janga la kushuka daraja.


Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England akitokea Genk ya Ubelgiji.
Tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ilipotangazwa kuwa ‘Samagoa’l atajiunga na Villa, Watanzania kutoka kona mbalimbali za dunia walikuwa wakisubiri kwa hamu kutimia kwa usajili huo.

Villa kwa sasa ipo nafasi ya 18 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England na  wamemchukua Samatta kwa lengo la kumaliza tatizo lao katika safu ya ushambuliaji msimu huu.

Leave A Reply