The House of Favourite Newspapers

Ni Man U au Arsenal leo?

0

EPL MASHABIKI wa soka duniani wanalisubiri kwa hamu pambano la leo la Ligi Kuu ya England kati ya Manchester United na Arsenal.

Mtanange huo unaotarajiwa kupigwa saa 11:05 leo jioni, Manchester United ndiyo wenyeji.

Timu hizo zinakutana wakati wenyeji Manchester United wakiwa na pointi 41 wakishika nafasi ya tano huku Arsenal wenye pointi 51 wakiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.

Katika mechi ya mwisho iliyozikutanisha timu hizo Oktoba 2015, Arsenal walishinda kwa mabao 3-0.

depay

Memphis Depay.

Man United leo watamtegemea winga wake mahiri Memphis Depay ambaye alionyesha kiwango cha juu katika mechi ya Kombe la Europa majuzi dhidi ya Midtjylland huku Arsenal wakifurahia kurejea kwa mshambuliaji wake anayeifahamu vizuri Man U, Danny Welbeck.

danny

Danny Welbeck.

Mechi 5 za mwisho kuzikutanisha timu hizo:

Arsenal 3-0 Manchester United, Oktoba 2015 (Premier League)

Manchester United 1-1 Arsenal, Mei 2015 (Premier League)

Manchester United 1-2 Arsenal, Machi 2015 (FA Cup)

Arsenal 1-2 Manchester United, Novemba 2014 (Premier League)

Arsenal 0-0 Manchester United, Februari 2014 (Premier League)

Arsenal-v-Manchester-United-Premier-League

Viwango vya timu hizo kwa sasa:

Michezo 5 ya mwisho ya Manchester United

Manchester United 5-1 FC Midtjylland (Europa League)

Shewsbury 0-3 Manchester United (FA Cup)

FC Midtjylland 2-1 Manchester United (Europa League)

Sunderland 2-1 Manchester United (Premier League)

Chelsea 1-1 Manchester United (Premier League)

Michezo 5 ya mwisho ya Arsenal

Arsenal 0-2 Barcelona (Champions League)

Arsenal 0-0 Hull (FA Cup)

Arsenal 2-1 Leicester (Premier League)

Bournemouth 0-2 Arsenal (Premier League)

Arsenal 0-0 Southampton (Premier League)

Leave A Reply