The House of Favourite Newspapers

Nido Kubwa Zamponza Mrembo, Ashushwa Kwenye Ndege Canada Akitaka Kwenda Marekani

0
MREMBO
Mary Magdalene (28); ni mrembo ambaye amekuwa gumzo duniani baada ya kudai kuponzwa na ukubwa wa matiti yake.

 

Mary Magdalene (28); ni mrembo ambaye amekuwa gumzo duniani baada ya kudai kuponzwa na ukubwa wa matiti yake (nido) na kushushwa kwenye ndege. Mary amedai kuondolewa utu wake wakati akiwa nchini Canada akitaka kwenda Marekani.

Hata hivyo, wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Marekani walipoulizwa wamekana madai ya Mary kwa kusema siyo kweli kwamba kifua chake au nguo alizovaa ndivyo vilimfanya ashushwe kwenye ndege.

Wafanyakazi hao wamesema kabla ndege haijaondoka, Mary alikuwa anapuyanga kukaa katika kila siti ndani ya ndege badala ya siti aliyopangiwa.

Pia wamesema mrembo huyo alionekana mtu ambaye ameshatumia kilevi au madawa na hakuonekana kuwa sawa ndipo wafanyakazi wakaingiwa na shaka kumtaka ashuke ambapo Mary alitii na kuondoka bila kuzua sokomoko lolote.

Mary kutoka Canada ana asili ya Uingereza na ni staa wa kwenye mitandao ya kijamii. Akiwa na miaka 20 hakuwa anavyoonekana sasa bali alianza kufanya sajari ili awe anavyotaka ambapo hadi sasa ametumia Euro 85,000 ambazo ni zaidi ya milioni 248 za Kitanzania kujibadilisha na kujikarabati mwili wake

 

Amesema kabla ya sajari hakuwa mbaya ila alikuwa na muonekano wa kawaida sana ambao hakuupenda na ulifanya asijiamini, lakini baada ya sajari kwa sasa anaupenda sana muonekano wake huo alionao
Aliwahi kunusurika kufa wakati akifanyiwa sajari ili kuongeza unene wa sehemu zake nyeti.

 

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

Leave A Reply