The House of Favourite Newspapers

Nigeria Yawatafuna Iceland Bao 2-0

NIGERIA ilizinduka leo kwa kuichapa Iceland mabao 2-0, matokeo ambayo yamefufua matumaini yao ya kutinga kwenye hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Dunia.

 

Winga wa Nigeria, Ahmed Musa ndiye aliibuka shujaa kwa kuifungia timu yake mabao mawili katika mchezo huo mkali wa Kundi D uliochezwa kwenye Uwanja wa Volgograd Arena.

Matokeo hayo yameifanya Nigeria iliyofungwa mechi ya kwanza na Croatia mabao 2-0, kufi kisha pointi tatu, ambapo inatakiwa kuifunga Argentina kwenye mechi yake ya mwisho ili ifi kishe pointi sita lakini ikitoka sare itafi kisha pointi nne na kufanya kulazimika kusubiri mato-keo baina ya Croatia na Iceland.

Matokeo ya jana, yameifanya Croatia yenye pointi sita baada ya kuiliza Argentina mabao 3-0 juzi, kujihakikisha tiketi ya mtoano kwani Argentina na Iceland hazina ubavu wa kufi kisha pointi sita baada ya kuwa na pointi moja kila mmoja kutokana na kufungana mabao 1-1 katika mchezo wa kwanza.

 

Iceland iliyotawala zaidi kipindi cha kwanza, ilipotea kipindi cha pili kwa Nigeria iliyoanza kwa kasi na winga wake mwenye mbio na chenga, Mussa kupachika bao la kwanza katika dakika ya 49 baada ya kuunganisha wavuni krosi ya Victor Moses.

Bao la pili la Mussa ndio lilikuwa kali zaidi ambalo alifunga katika dakika ya 75 baada ya kuambaa na mpira kutoka winga ya kushoto na kumtoka beki wa Iceland halafu akamlamba chenga kipa Hannes Halldorsson kabla ya kutulia na kupiga shuti lililotinga wavuni.

 

Mambo yalikuwa mbaya zaidi kwa Iceland ilipokosa penalti katika dakika ya 82 baada ya staa wake Gylfi Sigurdsson kupaisha. Katika hatua nyingine, Brazil nayo iliweka hai matumaini yao ya kuvuka Kundi E baada ya mabao yake ya dakika za majeruhi kuisaidia kuichapa Costa Rica 2-0 katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Krestovsky. Brazil iliyofi kisha pointi nne kutokana na kufungana 1-1 na Uswisi kwenye mechi ya kwanza.

Nigeria (3-5-2): Uzoho 8; Balogun 7, Ekong 7, Omeruo 7; Moses 6.5, Ndidi 6.5, Mikel 6.5, Etebo 7 (Iwobi 90), Idowu 6 (Ebuehi 45, 6); Musa 8.5, Iheanacho 7.5 (Ighalo 84)

Subs (not used): Ezenwa, Echiejile, Shehu, Nwankwo, Obi, Akpeyi, Onazi, Ogu, Awaziem

Scorers: Musa (49, 75)

Booked: Idowu

Manager: Gernot Rohr 7

Iceland (4-4-2): Halldorsson 6.5; Saevarsson 6.5, Arnason 6, R Sigurdsson 6 (Ingason 65, 6), Magnusson 6; Gislason 6, G Sigurdsson 6.5, Gunnarsson 6 (A F Skulason 86), Bjarnason 6; Finnbogason 6, Bodvarsson 6 (Sigurdarson 71, 6)

Subs (not used): Fridjonsson, A Gudmundsson, J B Gudmundsson, Schram, Runarsson, Eyjolfsson, O I Skulason, Hallfredsson, Traustason

Manager: Heimir Hallgrímsson 6

Referee: Matthew Conger 6.5

 

Comments are closed.