The House of Favourite Newspapers

NIKIFA WANANGU WASOMESHWE NA RAY

Steve Nyerere

CHEKESHAJI maarufu Bongo, Steve Nyerere amesema ingawa watu wamekuwa wakimkashifu kwa roho yake ya kujitolea na kusimamia misiba ya mastaa mbalimbali, lakini hatakoma kusimamia kwani ni kitu anachokifanya kutoka moyoni na kwamba ikitokea amefariki basi watoto wake wasomeshwe na msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Akipiga stori mbili tatu na Star Showbiz, Steve alisema kitendo hicho cha kusimamia misiba kimeweza kwa namna moja au nyingine kumfanya pia awe karibu na watu wazito nchini ambao wanamuunga mkono kwenye kujitolea kwake.

“Sitaacha kusimamia misiba ng’o, wanaosema waache waseme watachoka. Ninasimamia misiba kwa sababu ninafahamu na mimi ipo siku nitaondoka na watu watasimamia msiba wangu. Niseme tu wazi hata kama nikiondoka leo nataka Vincent Kigosi ‘Ray’ asimamie na kuwasomesha wanangu,” alimaliza Steve bila kutoa sababu hasa iliyofanya achukue uamuzi wa kutangaza hilo.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.