The House of Favourite Newspapers

Niliolewa na mganga kwa tamaa ya cheo kazini-35

0

ILIPOISHIA:

“Mmh! Temea chini babu umekamilika.”

“Basi mjukuu, kama babu hakufikishi kuna dawa nitakupa utamwekea kwenye chai, nakuhakikishia tabu zote zitaisha nawe utafaidi  kama wenzako.”

“Nitashukuru babu, lakini baada ya kurudi safari yangu, naogopa nikimwekea sasa hivi na mimi kuondoka nitakuwa nawatengenezea wengine huenda nikirudi asiwe wangu.”

SASA ENDELEA…

Basi ukirudi nitakupa.”

“Nitashukuru, ila bado nilikuwa na ombi moja.”

“Ombi gani mjukuu?”

“Ila babu usinielewe vibaya.”

Kwa kweli lazima niseme ukweli penzi alilonipa babu liliniridhisha akili na kutamani angalau nimpate kwa siku moja sehemu nzuri ili nikisafiri basi niwe mwepesi. Ilibidi nitengeneze mpango wa kumpeleka mjini kwa siku moja au mbili ili niweze kulifaidi penzi lake kwa kina. Niliamua mtoto wa kike kumvaa mzimamzima.

“Sema tu mjukuu wangu mimi na wewe!” babu alinitoa hofu.

“Babu najua mimi na wewe si wageni tena katika uhusiano?”

“Ndiyo najua, vipi unataka uwe mke wa tano?”

“Hapana babu.”

“Unatakaje?”

“Na…na…taka,” nilijikuta nikiingiwa na aibu ya kike kuishia kuuma kucha.

“Mjukuu sema tu yaani hujui wewe ni zaidi ya wake zangu sema chochote nitakusikiliza.”

“Nilikuwa nataka kama safari yangu itakuwepo uje tukae siku mbili kwangu.”

“Kuhusu safari yako ipo kama nilivyokueleza baada ya kesho kuikamilisha kazi iliyobaki. Jumatatu jioni kuna taarifa zitakufikia juu ya safari yako ila Jumanne utapata uhakika kamili.”

“Nitashukuru babu, kwa vile safari itakuwa Jumapili au Jumatatu najua nitapewa mapumziko ya kujiandaa na safari nataka nitafute hoteli nzuri nikae na wewe kwa siku mbili ili unimalize haja zangu kisha niondoke mwepesi mtoto wa kike.”

“Hakuna tatizo wewe tu.”

Kwa vile mazungumzo yetu tulikuwa tukitembea tulijikuta tukiingia maeneo ya nyumbani bila kujua.

“Basi babu usiniangushe nakutegemea wewe, penzi la kwenye majani limekuwa tamu vile vipi la hotelini tena kwenye kitanda kipana si ndiyo nitasahau safari?”

“Walaa, najua una kutu kwa siku mbili nitaitoa yote. Dozi  nitakayokupa itakufanya usiwaze mapenzi mpaka unarudi.”

“Unaona babu, hiyo ndiyo naitaka au tufanye siku tatu?”

“Hizo mbili zinatosha si unajua hali aliyonayo shoga yako hapendi niwe mbali kwa kipindi hiki.”

“Sawa, lakini usipozimaliza sikuruhusu uondoke.”

Tulikuwa tumekaribia nyumbani, tulibadili mazungumzo, kwa vile ulikuwa usiku sana nilikwenda kwenye chumba nilichoandaliwa na kulala kuitafuta siku ya pili. Usiku ulikuwa mrefu kwangu niliwaza mengi juu ya uwezo wa kimapenzi wa babu yule ambaye ukimwangalia vibaya utasema atakufia kifuani.

Nilifurahi kukubali ombi langu la kuja mjini kunipa raha kwa siku mbili kabla ya safari japo bado sikuamini kama safari kwa upande wangu ilikuwepo. Usingizi ulivyonichukua sikujua nilishtushwa na sauti ya Rose aliyeniamsha. Macho yangu yalikutana na mwanga mkali kuonesha kumekucha muda mrefu.

“Vipi shoga mpaka asubuhi unakoroma jana ulichoka sana?”

“Kiasi sema tumerudi muda mbaya.”

“Kwa hiyo unaondoka saa ngapi?”

“Siondoki leo.”

“Kwa nini?”

“Shughuli tulidhania ndogo kumbe nzito, jana hatukumaliza tunamalizia leo.”

“Pole shoga ndiyo kutafuta huko usikate  tamaa.”

“Nashukuru shoga kwa moyo wako,” nilimshukuru Rose bila kujua kwenye kibuyu chao cha asali nami nimetia mkono.

Niliamka kuoga na kukuta kifungua kinywa kimeshaandaliwa, niliungana na wenzangu kupata kifungua kinywa. Baada ya kufungua kinywa nilijumuika na wenzangu kuzungumza mawili matatu. Mzee Sionjwi alituaga anakwenda porini kufuata dawa ya kazi ya usiku.

Ajabu wakati babu anaondoka nilimsindikiza kwa macho huku hali yangu ikibadilika na kutamani kitu kutoka kwake. Lakini nilijizuia kama asingekuwa ana wake ningemuomba nifuatane naye ili akanipe raha tena.

angalau cha majanini ili usiku kwenye kazi  tusiingie majaribuni na kuharibu tena tiba.

                                                          ***

Usiku kama kawaida baada ya chakula cha usiku na kupumzika kidogo safari ya mzimuni ilianza. Nilibeba vitu kama nilivyobeba jana yake ila tuliongeza na kuku mwekundu ambaye tulikwenda naye kwa ajili ya kuuomba  mzimu msamaha kutokana na uchafu wetu wa jana yake.

Tulipofika, nilivua nguo zangu zote na kujifunga upande wa kanga na yeye alijifunga kipande cha shuka nyeupe. Alimchukua kuku na kusogea karibu ya mti ule mkubwa na kusema kwa sauti ya juu.

“Mzimu najua jana uliondoka kwa hasira, leo nimekuleta zawadi nzuuuuri, naomba uje uchukue.”

Alimweka kuku juu ya jiwe lililokuwa mbele ya mti mkubwa, mara ghafla nilisikia mtikisiko ukifuatiwa na upepo  mwanana. Ghafla niliona majani yakizunguka kama kimbunga na kuelekea kwenye lile jiwe na kuzunguka kwa muda kisha ulipanda juu kuelekea juu ya mti ule mkubwa.

Ajabu ya Mungu kuku yule hakuwepo kuonesha mzimu ulikuja kama kimbunga na kuondoka na yule kuku.  Baada ya muda hali ilitulia na kutokea mguno mzito kisha pakawa kimya.

Mganga alichukua usinga wake na maji ya dawa na kuanza kunyasia kila kona na kusema:

“Asante mzimu, asante kwa kukubali ombi letu na kutuhakikishia kazi iliyofanyika imekwenda vizuri.”

Baada ya kusema vile aliweka  dawa kwenye maji yaliyokuwa kwenye beseni pamoja na majani ya kujisugulia. Alinieleza nijimwagie maji na kujisugua na majani kisha nijimwagie tena maji kuondoa uchafu na baada ya zoezi hilo aliniwekea kipande cha shuka nyeupe pembeni ili nijifunge.

Ajabu ya Musa baada ya kunitayarishia  kila kitu aliondoka na kuniacha peke yangu na yeye kwenda kuendelea na mambo mengine na kuniomba nikimaliza nimjulishe ili tuendelee na zoezi lingine.  Sikutaka kuhoji ya jana yake na ya siku ile.

Nilifanya kama nilivyoelekezwa kwa kujimwagia maji na kujisugua mwili mzima ilikuwa tofauti na jana yake kujisugua kiungo kimojakimoja na kujimwagia maji na kuhamia kingine lakini siku ile baada ya kujimwagia maji mwili mzima nilitakiwa kujisugua na majani yale mwili mzima kisha kujimwagia maji tena baada ya hapo zoezi lile linakuwa limekwisha.

Baada ya kumaliza zoezi  nilivua kanga iliyokuwa imetota kwa maji na kujifunga kipande cha shuka nyeupe kisha nilimwita  babu kuwa nimemaliza.

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia hadithi hii ya kusisimua katika Risasi Jumamosi siku ya Jumamosi.

  Itaendelea Risasi Jumamosi.

Leave A Reply