The House of Favourite Newspapers

NISHA ATAMBA KWA MAKALIO, MATITI !

Salma Jabu ‘Nisha’

BAADA ya kuweka picha mtandaoni na kushambuliwa kwamba amevaa kigodoro, msanii wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kueleza kuwa anajikubali sana kwa makalio yake na matiti na hakuna staa anayemfikia.

Nisha aliiambia Za Motomoto News kuwa alichukua futi na kujipima makalio na matiti yake na kuwaangalia mastaa wanawake wenzake ambapo aligundua kwamba anawazidi sana na anamshukuru Mungu kwa kumpa zawadi hizo nzuri za kudumu.

“Najikubali mwenyewe hata kama watu wakinishambulia, sijavaa kigodoro kwenye picha niliyoweka mtandaoni bali ni jinsi Mungu alivyonijaalia na hakuna staa wa kike anayenifikia, najivunia sana kwa kweli,” alisema Nisha.

Comments are closed.