The House of Favourite Newspapers

Nisha Kula Futari na Watoto Yatima

0

nisha (1)

Msanii wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’ akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), kushoto kwake ni mmoja watoto yatima.nisha (2)

Mkutano ukiendelea.nisha (3)

Nisha akitoa ufanunuzi wa jambo.nisha (4)Nisha akijibu maswali ya wanahabari.

MSANII wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ kupitia Kampuni yake ya Nisha’s Film Production anatarajia kuwakutanisha watoto waishio katika mazingira hatarishi wanaoishi Dar es Salaam kwa ajili ya futari, Juni 26, mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Azania, Upanga jijini hapa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Nisha amesema kuwa lengo kubwa la kula futari na watoto hao wanaishi katika mazingira hatarishi ni kuwapa faraja na kusikia changamoto zinazowakabili.

Alisema wito wa dini yake ya Kiislamu hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wanapaswa kutoa zaka pamoja na kuonyesha upendo kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu hasa watoto yatima, walemavu, wanaoishi mitaani pamoja na watoto wenye ualbino kwa kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali ambazo zinaweza kuwa ni sehemu ya faraja kwao.

Alifafanua kuwa muda wa futari hiyo utakuwa ni kuanzia saa 10 jioni hadi saa mbili usiku ambapo wanatarajia kuwepo viongozi mbalimbali wa serikali kama Makamu wa Rais Bi Samiah Hassan Suluhu, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, viongozi mbalimbali wa dini, wasanii na watu mashuhuri.

Vilevile alitoa wito kwa watu wote wanaoishi katika mazingira hayo ili waweze kufika na ambao wapo katika vituo vya mbali waweze kuwasiliana kwa namba za simu +255 676894246/ 0789586057 .

Nisha’s Film Production iliyo chini ya Mkurugenzi Salma Jabu (Nisha) ni watengenezaji wa filamu pamoja na uandaji wa matamasha mbalimbali ya wasanii ambayo yanalenga kuelemisha na kuburudisha jamii.

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave A Reply