The House of Favourite Newspapers

Niyonzima Apewa Ndinga Mpya Simba

0
Haruna Niyonzima.

BAADA ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon ya Rwanda kwenye Simba Day, kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima ametunukiwa gari mpya aina ya Toyota Brevis, ambayo atakuwa akiitumia kwa sasa.

 

Niyonzima aliyejiunga na Simba katika dirisha kubwa la usajili akitokea Yanga, Jumanne ya wiki hii aligeuka lulu kwa mashabiki na viongozi wa klabu hiyo baada ya kuingia uwanjani kipindi cha pili cha mchezo huo na kuonyesha kiwango kikubwa.

Kikizungumza na Championi Ijumaa, chanzo makini kutoka ndani ya timu hiyo kimeweka wazi kuwa tayari Simba wamempatia gari hiyo ikiwa ni moja ya kuonyesha mapenzi yao kama walivyomuahidi katika mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo ikiwa pamoja na kumpangia nyumba mpya ya kuishi.

 

“Juzi (jana) Niyonzima alikabidhiwa gari lake jipya aina ya Toyota Brevis, baada tu ya kuonyesha uwezo dhidi ya ndugu zake Rayon kwenye mechi ya Simba Day.

“Kwenye mkataba wake wa kuitumikia Simba alipotoka Yanga aliahidiwa kupangishiwa nyumba na kupewa usafiri mpya ambapo juzi (jana) ndiyo alikabidhiwa rasmi gari la kutembelea,” kilisema chanzo.

 

Aidha, kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga,

Niyonzima amesema ikiwa atafanikiwa kufunga bao dhidi ya timu yake hiyo ya zamani atashangilia lakini atafanya hivyo kwa heshima ili kuwaaga vizuri mashabiki wa timu hiyo.

Musa Mateja na Ibrahim Mussa | CHAMPIONI IJUMAA |DAR

 

Uchambuzi Mahsusi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa TFF

Leave A Reply