The House of Favourite Newspapers

Nkomola Aanza Rasmi Mazoezi Yanga

 

 

Mshambuliaji Mpya wa Yanga, Yohana Nkomola, Akiwa Mazoezini

MSHAMBULIAJI  mpya wa Yanga, Yohana Nkomola, ameungana rasmi na wachezaji wa Yanga kwenye mazoezi yao baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya taifa, Kilimanjaro Stars,  ikiwa ni siku moja baada ya kutua nchini akitokea kwenye kikosi hicho.

Straika huyo ambaye tangu asajiliwe na Yanga hakuwahi kufanya mazoezi na kikosi hicho kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, leo kwa mara ya kwanza amefanya mazoezi ya pamoja na wenzake huku akikutana uso kwa uso na washambuliaji wenzake kama Amissi Tambwe  na kiungo Papy.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina na Msaidizi Wake, Shadrack Nsajigwa, Wakiwaonyesha Mfano Wachezaji Wao

Yanga imeendelea na mazoezi ya uwanjani leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar kwa ajili ya maandalizi ya michuano  ya FA na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea karibuni.

Na Musa Mateja/GPL

 

Comments are closed.