The House of Favourite Newspapers

Video: NMB Yazindua ‘Fanikiwa Account’ Kuwasadia Wafanyabiashara

0
Mkurugenzi Mtendaji wa wa NMB, Ineke Busemaker (katikati) akizungumza jambo kuhusiana na NMB FANIKIWA itakavyowawezesha wafanyabiashara wadogo.

Benki ya NMB, imezindua rasmi huduma yake mpya ya Fanikiwa Accounts ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo kupata mikopo ya biashara itakayowasaidia kukuza mitaji yao na kuboresha huduma kwa wateja.

Uzinduzi wa huduma hiyo umefanyika makao makuu ya benki hiyo ya NMB, Posta jijini Dar es Salaam.

Fanikiwa Account, humuwezesha mfanyabiashara kutenganisha vizuri mapato ya biashara na kutunza mtaji, hivyo kuwa na uhakika wa kufanya biashara hata katika wakati mgumu wa kiuchumi.

Pia ni rahisi kufungua, pesa zinazowekwa benki zinakuwa na riba nzuri kwa mfanyabiashara, tofauti na akaunti nyingine.

Leave A Reply