The House of Favourite Newspapers

Nuh Mziwanda na Shilole Wadaiwa Kurudisha Penzi Lao

nuh-7 MSANII wa kizazi kipya aliyetambulika kupitia wimbo wake wa ‘Msondo Ngoma’ uliotolewa na studio za ‘Mazooh Record’ jijini Dar es Salaam, Nuh Mziwanda,  amekanusha habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa alikuwa na mpenzi wake wa zamani, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, jijini Mwanza siku mbili zilizopita.nuh-1

Akizungumza kupitia kipindi cha Planet Bongo cha kituo cha televisheni cha EATV,  Mziwanda amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa alisikia Shilole alikuwa jijini Mwanza kwenye klabu ambayo yeye alikuwa anafanya shoo lakini hawakuonana.

nuh-19“Siwezi kumkataza mtu kuingia mahali popote, hilo ni jambo la kawaida.  Niliambiwa yupo humu mjini ‘so’ sikujali maana mimi nilienda kufanya kazi na yeye alikwenda kufanya kazi kimipango yake. Kwa hiyo hayo maneno mengine yanayoongeleka mimi mwenyewe siyajui, mimi nimekuja Mwanza kutafuta pesa,” alisema. nuh-2“Mimi nimeoa najiheshimu, siwezi kufanya vitu ambavyo si vya maadili au ambavyo sitakiwi kuvifanya.  Kilichonileta Mwanza ni kufanya shoo na kufanya makubaliano na kusaini mkataba wa shoo yangu nyingine itakayofanyika Dar es Salaam, ” alisisitiza.   nuh-8

Pamoja na hali hiyo ya sintofahamu kuhusu wawili hao waliowahi kuwa wapenzi,  hivi sasa Shilole anatajwa kuendelea kupenda vijana wadogo kwani baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Mtoto Mdogo Mdogo’ alionekana akitoka na ‘kadogoo’ mmoja anayejulikana kwa jina la Hamadai.

 

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.