The House of Favourite Newspapers

Nyama Nyekundu Inavyosababisha Kisukari, Moyo, Kansa

0

NILIWAHI kuandika kuhusu madhara ya nyama nyekundu ingawa watu wengi hawajui kwamba ina hatari zake. Kutokana na wengi kupenda nirudie kuandika madhara ya nyama leo tutangalia madhara yake mwilini kwa mlaji. Wapenda nyama za mishikaki, mapande ya kuchomwa, rosti, supu, na wale wanaotumia kama kitoweo wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupatwa na saratani na ugonjwa wa moyo.

ULAJI WA NYAMA WA FAIDA

Ulaji wa nyama nyekundu wenye faida kwa mwili wa binadamu ni ule unaozingatia kiasi na aina ya nyama. Wenye hatari ni wale wanaokula kuanzia kiasi cha kama robo kilo kila siku lakini wanaokula kiwango kidogo hawako hatarini sana na badala yake watapata virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye hiyo nyama. Nyama inayopendekezwa ni steki isiyo na chembe ya mafuta (lean meat) na itakayoliwa kwa kiasi kidogo kwa sababu ina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa wasichana na wanawake wanaotarajia kuzaa. Pia nyama ina Vitamini B12 ambayo husaidia utengenezaji wa vinasaba (DNA) na hujenga mishipa na seli za damu. Hali kadhalika kuna madini ya zinki ambayo husaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa kinga ya mwili. Bila kusahau kuwa nyama ina protini ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa mifupa na misuli katika mwili wa binadamu. Nyama nyekundu ni zile zenye
kumbukumbu kabisa. Wanasayansi wanasema protini inayopatikana kwenye nyama iitwayo Tau and beta-amyloid huharibu mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia kwa ugonjwa huu.

NYAMA NYEKUNDU NA UGONJWA WA MOYO

Hatari nyingine ni ya kupata magonjwa ya moyo. Nyama ina kitu kinaitwa lehemu kitaalamu cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri hata kwenye moyo. Hii husababisha viungo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kufanya kazi yake sawasawa. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwenye nyama, ni hatari sana kwani nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi.

KANSA YA UTUMBO

Nyama nyekundu ikiliwa inakaa saa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine.Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.

UGONJWA WA KISUKARI

Utafiti mpya Marekani umeonyesha kwamba watu wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo (cohort studies); watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula, hivyo ni muhimu kuiepuka.
rangi nyekundu kabla ya kupikwa ambazo ni za ng’ombe, mbuzi, kondoo nyati, swala, nyumbu na wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne wakiwemo nguruwe ambao baadhi ya watu wanajidanyganya kuwa ni wa nyama nyeupe, kumbe weupe ni wa ngozi tu.

NYAMA NYEUPE

Nyama nyeupe ni zile ambazo zina rangi nyeupe ndani kabla ya kupikwa mfano kuku, bata, samaki aina zote, mbuni na wanyama wote wanaotembea kwa miguu miwili. Nyama nyeupe ni salama sana kuliko nyama nyekundu.

MADHARA YA NYAMA NYEKUNDU

Ulaji wa nyama nyekundu una madhara makubwa sana kuliko ulaji
wa nyama nyeupe, hata hivyo, watu ambao hawali nyama kabisa wako mbali sana na hatari hizi nane nitakazozitaja. Mlaji wa nyama ana hatari ya kupata ugonjwa wa alzheirs disease; huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza

UGONJWA WA KISASA

Minyoo inayopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Hali hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive vizuri. UNENE ULIOPITILIZA Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo, mfano kwenye nyama ya nguruwe. Unene na kitambi ni hatari sana kwani husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye suala la unene.

NYAMA YA KUKU

Nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa hapa Tanzania ni kuku wa kisasa, wanakuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji. Nyama ya kuku inayoshauriwa kuliwa ni ya wale wa kienyeji.

MAGONJWA YA WANYAMA

Kuna magonjwa mengi ya wanyama ambayo ni hatari kwa binadamu. Yameua watu wengi na mengine hayatibiki kabisa, mfano mafua ya ndege, ebola ambao pia virusi vyake huishi kwenye nyama ya popo. Mlaji wa nyama ndiye hupata magonjwa hayo kama mnyama ana virusi vyake. USHAURI Wote wenye matazizo la moyo, presha, kisukari na kansa wanashauri kuacha kula nyama nyekundu kabisa kwani ni hatari kwa afya zao. Makala haya imeandaliwa na Mtaalamu wa Lishe, Mandai Abdallah pia soma makala za afya kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda kila Jumatatu.

 

Leave A Reply