The House of Favourite Newspapers

NYANGWINE AWAASA WAHITIMU KIDAO CHA SITA KUSOMA KWA BIDII

Mbunge wa zamani wa Tarime, Nyambari Nyangwine akizungumza jambo.

 

Mbunge wa zamani wa Tarime, Nyambari Nyangwine ambaye pia ni mwandishi wa vitabu vya riwaya leo amewaasa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Kibaha, kusoma kwa bidii ili kufanikisha ndoto yao hapo baadaye.

Nyambari akitoa vyeti kwa wahitimu wa Kidato cha sita Shule ya Sekondari Kibaha.

” Ningewasihi sana wanafunzi hakuna silaha kubwa kama kujitahidi kwenye masomo ndio unaweza kupenya popote lakini bila elimu ni bure tu,na ni vyema mkatetema na masomo zaidi” alisema Nyambari ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.

…Nyambari akiendelea kutoa vyeti kwa wahitimu
Akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo alipowasili kwenye hafla hiyo.
Vijana machachari wa Scout wakimvisha Skafu Mgeni rasmi.
Nyambari Nyangwine akizungumza jambo kabla ya kufungua boksi kwa ajili ya harambee ya kuchangia ujenzi wa  ukumbi wa shule ya Sekondari Kibaha.

Comments are closed.