Nyumba ya Mchungaji Yachomwa Moto Kisa Maiti Kukutwa Ndani

VIJANA wenye hasira kali wameichoma moto nyumba ya mchungaji wa kanisa mjini Adebun huko Ado-Ekiti nchini Nigeria baada ya mtoto mwenye umri wa miaka saba kukutwa amefariki ndani kwake.

 

Taarifa zinadai kuwa mtoto wa kike huyo aliyefahamika kwa jina la Demilade, alikuwa amepotea kwa saa kadhaa, kabla ya mwili wake kukutwa ndani ya nyumba ya mtumishi huyo ambaye ni jirani yao.

 

Kupotea kulikuja baada ya kuagizwa na wazazi wake, ikielezwa kuwa aliingia ndani kwa mchungaji kumfuata mtoto mwenzake ambaye ana tatizo la afya ya akili.

 

Ulipofanyika msako kwa kushirikiana na majirani, ambapo polisi walishafikishiwa taarifa, ndipo mwili wa Demilade ulipopatikana kwenye nyumba ya mchungaji huyo.


Toa comment